
TWENDE
TWENDE is a Christian magazine for children and youth. Through this magazine we want to afflict children and youth gospel of eternal life in Jesus Christ. It has cartoons, stories, games, devotions and Biblestories.
TWENDE comes out four times a year.
Price: 500 Tsh pr copy
Fore more information, contact us:
TWENDE P.o. Box 2696, Arusha, Tanzania
E-mail: layout.somabiblia@gmail.com
TWENDE ni gazeti la Kikristo kwa Watoto na Vijana. Kupitia gazeti hili, tunataka kufundisha Watoto na vijana Injili ya uzima wa milele ndani ya Yesu Kristo.
TWENDE inatolewa mara nne kwa mwaka.
Bei: 500 Tsh kwa nakala moja
Wasiliana nasi:
TWENDE 0759 544 917 , P.O.Box 2696, Arusha, Tanzania
Barua pepe: layout.somabiblia@gmail.com
Twende toleo no. 2,2022
Katika toleo hili tunajifunza juu ya 'Kukaza Mwendo'. Kupitia makala mbalimbali tutajifunza maana hasa ya kukaza mwendo kwenda Mbinguni, na zaidi tutaelewa kuwa sisi ni washindi tunaoweza kuzishinda changamoto za dunia hii kwa sababu yupo mmoja ambaye anatuwezesha kushinda tukiwa naye.
Linapatikana kwa Tsh. 500 tu.
Twende toleo no. 2, 2020
Katika toleo hili utajifunza kuhusu kupata Mia kwa Mia. Utagundua kuwa yupo mmoja anayetafuta kutushindia kwa asilimia Mia kwa Mia wakati sisi wenyewe hatuwezi. Kuna simulizi nzuri ya moja ya mifano yake inayothibitisha anataka kupata mia kwa mia.
Karibu kusoma! Linapatikana dukani Soma Biblia
Twende toleo no. 4, 2019
Mtoto mwenzangu, toleo hili lina habari njema kuhusu maisha yetu ya sasa na ya baadaye. Tutambue kwamba tukiwa ndani ya Yesu tutakuwa salama sasa na siku zijazo, na hata tukifa tutaenda kuishi na Yesu kwa furaha mbinguni.
Karibu usome!
Twende toleo no. 2, 2019
Umewahi kusikia mtu akisema, “Mimi ni mwanafunzi wa Yesu”? Au, “Mimi ni mtoto wa Yesu? Au, “Mimi ni mtumishi wa Yesu? Je, ana maana gani hasa?
Soma makala za gazeti hili upate ufafanuzi mzuri kuhusu swali hili.
Twende toll no. 4, 2018
Amani ni kuwa na hali ya usalama uletao raha ya kufanya kazi zetu na raha moyoni. Kusiwe na woga moyoni mwako, wala ugomvi kati yako na mwingine au vita kati ya nchi na nchi, kwa sababu amani ipo. Amani yetu sisi Wakristo inatoka wapi?
Karibu usome toleo hili ujue zaidi maana ya amani.
Twende toleo no. 2, 2018
Soma makala na vibonzo katika toleo hili ujifunze zaidi juu ya ushindi katika Kristo Yesu.
Twende toleo no.4, 2017
Kumsifu Mungu ni kwa kumuinua juu, kumshukuru, kumpazia sauti, kumfanyia shangwe na kujishusha chini yake kwa unyeyekevu. Soma toleo hili ujifunze zaidi maana ya sifa.
Twende toleo no. 2, 2017
Maombi ni kuongea na Mungu ili kumkaribisha Yesu ndani yetu. Toleo hili limefafanua zaidi maana ya maombi.
Twende toleo no. 1,2022
Toleo hili linafafanua jinsi kuu ya kuondokana na mashaka, nayo ni kumfuata Yesu. Yeye ni Mungu pamoja nasi. Kupitia makala mbalimbali, michezo na katuni, utajifunza na kuelewa zaidi habari hii njema.
Karibu kununua dukani Soma Biblia kwa 500/= tu.
Twende toleo no. 1, 2020
Mtoto mwenzangu katika toleo hili tutajifunza juu ya sauti ya Mungu. Je, unajua Mungu anatuita, na jinsi tunavyoweza kuisikia sauti yake na kuifuata?
Karibu kusoma toleo hili uelewe vizuri zaidi.
Twende toleo no. 3, 2019
Hebu fikiri kidogo kwamba sote tume-tenda dhambi. Hivyo hatukustahili kitu kwa Mungu. Lakini alifanyaje? Alimtuma Yesu atukomboe na kutufanya watoto wake.
Habari hii njema tunafafanua zaidi katika toleo hili.
Twende toleo no. 1, 2019
Karibu usome gazeti hili linalofafanua kuhusu safari yetu ya kwenda mbinguni.
Twende toleo no. 3, 2018
Kwetu sisi Wakristo uvumilivu ni hali ya kuendelea kumpenda na kumcha Mungu wakati wote, hasa pale tunapokuwa kwenye hali ya shida na mahangaiko. Soma toleo hili ujifunze zaidi.
Twende toleo no. 1, 2018
Katika toleo hili tunafafanua zaidi jinsi mtu anavyotoka katika utumwa na kuwa huru kweli pale anapomkaribisha Yesu aingie maishani mwake ili kuwa mwokozi na bwana wake.
Twende toleo no. 3, 2017
Neema ni zawadi, tena zawadi kutoka kwa Mungu.Toleo hili lina mambo mzuri yanayofafanua zaidi juu ya neema.
Twende toleo no. 1, 2017
Toleo hili linafafanua kwa namna rahisi ili wote waelewe maana ya Yesu kuwa Mwanadamu kweli na Mungu kweli.
Twende toleo no. 4, 2016
Yesu ni mfalme! Na yeye pia anataka kuongeza ufalme wake. Lakini njia yake ni tofauti kabisa na hizo za wafalme wa duniani. Karibu ujifunze juu ya Mfalme wa ajabu.