Kumbukumbu ya ”Mzee JJ”, Jon Jøssang 30.10.1926-30.12.2016
Anne Gihlemoen
Kwa majonzi makubwa tunasikitika kutangaza kifo cha mwanzilishi wa Scripture Mission, Mzee Jon Jøssang. Mzee Jøssang amefariki tarehe 30 desemba, 2016 huko Norway alipokuwa akiishi na familia yake. Jøssang amefariki akiwa mzee wa umri wa miaka 90.
Utawezaje kuyaelezea maisha ya thamani kama yalivyo ya Mzee JJ? Wasifu wake hauna mwisho. Alikuwa mcheshi, mthubutu na bila hofu. Alikuwa akimwamini Yesu kweli, lakini sio bila udadisi, na labda hilo ndilo lililofanya mahubiri yake kuwa halisi na ya kuaminika. Yeye na mke wake waliweza kutengeneza mambo makubwa kutoka hata kwenye kile kilichoonekana kama uchafu, jambo lililowapa haki ya kuishi kwenye mipango ya Mungu juu ya maisha yao. Lakini lipo jambo moja kutoka kwenye maisha ya JJ ambalo kweli linatupa picha ya jinsi alivyokuwa, na kwa nini aliweza kufanya yale aliyoyafanya: Siku zote aliongozwa na swali “Jinsi gani utamuongoza mtu kwenda Yesu”.
Jon Jøssang, alifahamika sana kama JJ, aliitwa na Mungu mapema wakati wa ujana wake kuwa Mmishenari. Alifika Tanganyika kwa mara ya kwanza mwaka 1954 kama Mmishenari kupitia Norwegian Lutheran Mission. Alifanya kazi kwa miaka mingi huko Dongobesh na Kansay wilaya ya Mbulu. Alitumikia, kama alivyojiita “Jack of all trades” (mchapakazi); Mjenzi mtumishi, mashine ya gari, dereva, mhubiri na mwandishi. Alijenga mashule na makanisa na ilikuwa sehemu ya hospitali ya Lutheran Haydom. Na pia alikuwa mhubiri siku za jumapili. Alimuoa Kjellaug mwaka wake wa kwanza huko Kansay, Mama mwenye moyo safi kutoka Norway ambaye alikulia huko China kama mtoto wa Mmishenari. JJ na ”Memsab” (kama JJ alivyokuwa akimwita mkewe) ni miongoni mwa mashuhuda wa matokeo ya kihistoria nchini Tanzania: walikuwepo wakati wa ”Uhuru”, walisikia hotuba ya Nyerere na kuona Tanganyika na Zanzibar zikiungana kuwa Tanzania.
Lakini mwongozo wa Mzee Jøssang, ulianza usiku mmoja ambapo alishindwa kulala. Aliwaona watanzania wengi sana wakibatizwa, lakini hakuwa na chochote kilichoandikwa kuwasaidia waliobatizwa kuendelea kujifunza kuhusu Imani yao mpya. Kwa hiyo yeye pamoja na Mmishenari mwenzake kutoka Norway, Ingebjorg Boe, walitengeneza vijarida viwili (”Hubiri Habari Njema” na ”Tufundishe kwa Furaha”) kuwasaidia wainjilisti na walimu wa shule ya jumapili kwenye kazi zao. Tunajua, mipango ya Mungu nimikubwa kuliko yetu sote, na vile vijarida viwili vilitengeneza mwanzo wa mambo makubwa zaidi ya yale yaliyofikiri JJ. Kwa sababu ya kukosa usingizi siku nyingine miaka ya 1971, wakati JJ na Kjellaug`s muda wao Tanzania ukiwa umekaribia kwisha, JJ alisikia jina ”VOI”. Na siku moja alipokuwa na shughuli zake huko Moshi, JJ alifikiri sio mbali sana na Voi, kwa hiyo aliruka mipaka na kuingia katika mji mdogo nchini Kenya, VOI. Huko voi, JJ alikuta shamba la zamani la katani lenye majengo mawili yaliyochakaa. JJ alikutana na wamiliki na akaruhusiwa kupanga eneo hilo kwa gharama ndogo sana. Kwa hiyo baada ya mapumziko kidogo huko Norway, JJ na Kjellaug na watoto wao wawili, walihamia Voi.
Huko Voi JJ alianza kufanya kile Mungu alichoweka ndani yake: kama kufundisha Biblia kwenye shule mbili za sekondari, na kutembelea kila wakati gereza la Manyani na kuhubiri huko. Kisha JJ aligundua basi lililokuwa likisafiri maeneo mengi ya Afrika mashariki na lilikuwa linakituo hapo Voi pia, na alianza kupeleka vijarida kwenye kituo cha basi. Vijarida 96000 vilikuwa vikisambazwa kwa watu kwa mfumo huo! Na JJ aligundua nafasi kubwa ya kueneza Injili kupitia kituo cha basi. Lakini alihitaji msaada. Haikuwa tatizo! JJ alikuwa mtu anayekutana na wasaidizi kila mahali! Alichohitaji ni kama vile Barnaba alivyosema kwa Saul mara ya kwanza kukutana ”Umemuona Yesu?”. Hata mtu awe mwanglikan, baptisti au presbyterian haikuwa na maana kwa JJ. Swali moja lilikuwa: ”Je wenzangu wanaye Yesu moyoni mwao?” Jambo ambalo lilimpeleka kwa watu wazuri wa Mungu, kwa mfano Josefu ambaye JJ alimwajiri kuuza Biblia, vitabu na vijarida katika kituo cha basi kwa kuweka meza ndogo. Wakati biashara ilipokuwa walifungua duka ndogo la vitabu.
Pia nafasi ya kuwaongoza watu kwa Yesu kupitia mawasiliano na mafunzo ilikuwa jambo ambalo JJ alilifanya. Aliandika kijitabu kidogo na rahisi lakini cha thamani kwa lugha ya Kiswahili kilichoitwa ”Dini na Maisha” (Faith and Life). Kitabu hiki kilitengenezwa kwaajili ya mafunzo ya Biblia, na hata leo kinatumiwa na Soma Biblia kama kifaa kwenye masomo ya Biblia kwa njia ya posta na ni moja ya vitabu maarufu sana vya Soma Biblia. Pia ”Badala ya” ambacho kwa maana rahisi kinaeleza jinsi Yesu alivyolipia deni ya makosa yetu, kilienea kule Voi na kuwa kitabu maarufu na hata sasa bado kinaendelea kwenda sokoni.
Mwaka 1976 JJ aliweza kusajili NLM’s kile kilichokuja kuwa idara ya machapisho nchini Kenya ”SCRIPTURE MISSION”. Akiwa ofisini Nairobi wakati wa usajili wa kazi za kimisheni, JJ aliambiwa ”lilikuwa ni jina nzuri sana!” .
Kazi za maandiko za JJ`s lilipanuka na wamishenari wengi walikuja. Tawi moja ya Scripture Mission ilifunguliwa katika eneo la NLM huko Nairobi. Magazeti mawili yalianzishwa, RIZIKI kwaajili ya wainjilisti na wachungaji, na ”The Brief” kwaajili ya wanafunzi. RIZIKI hata sasa ni gazeti nzuri na linasambazwa kwa wingi zaidi! Kazi iliendelea kukua, na nguvu kubwa iliwekwa kwenye vyombo vya mawasiliano, hata station ya radio ilijengwa kule Voi na Wazee Jossang waliihamisha ofisi ya maandiko kwenda Wundanyi kule Taita Hills. Hapa walijenga nyumba yao na eneo la kazi kwa miaka mingi, wakipaita Hebron. Shauku ya maandiko kufika mbali na kuenea Afrika mashariki yote, ilizaa Scripture Mission Tanzania mwaka 1985, wakiwa wamishenari kutoka Norwegian walioamua kuipeleka mbele kazi ya JJ.
JJ na Kjellaug waliendeleza kazi ya maandiko huko Wundanyi mpaka mwaka 1993, hapo walistaafu. Pamoja na kwamba wapendanao kama JJ na Kjellaug hawawezi kuondoka Afrika Mashariki kama hivyo, wao waliendelea kuishi kwa muda kidogo mpaka 2006 ambapo afya ya JJ ilianza kutetereka baada ya kugundulika ana ugonjwa wa Parkinson. Lakini pia wakati wa miaka yake kumi iliyopita, JJ aliendelea kufuatilia kazi za Scripture Mission kwa ukaribu, ikiwemo kuungana kwa Scripture Mission na Soma Biblia mwaka 2015.
Leo hii, Biblia, Vitabu vya Kikristo, Majarida, vijarida na magazeti yanasambazwa kila siku nchini Tanzania kupitia Soma Biblia magari ya usambazaji au maduka ya Soma Biblia. Tunashukuru sana kwa kazi aliyoianzisha JJ, ikiwa chanzo kikuu cha kuwepo kwa kazi yetu: Jinsi gani tutaendelea kuwaongoza watu kwenda kwa Yesu?
Anne Gihlemoen