FIKIA MAISHA
Cathbert Msemo
Programu mpya ya vijana
Mambo vipi! Vijana, angalieni hapa, tumepata kifaa. Soma Biblia pamoja na Biblica Kenya tumezindua programu mpya ya vijana ijulikanayo kama FIKIA MAISHA. Sasa mambo ni poa kabisa.
FIKIA MAISHA ni kitabu cha Agano Jipya kilichoandaliwa kipekee kwa ajili ya vijana. Kina mijadala ya changamoto zinazowakabili vijana. Programu ina sehemu kuu nne ambazo ni AMINI, KUA, ISHI na BADILIKA. Kitabu kina maswali ya uchokozi ili kijana aweze kujadili na kudadisi. Mifano: Unataka kuishi? Unataka kupata nguvu? Unataka kuishi kikamilifu? Je wataka kubadili ulimwengu? Maswali haya yanafuatiwa na mada mbalimbali kwa ajili ya majadiliano na zote huongozwa na vifungu vya Biblia.
Kama wewe ni kijana na kutaka kujua zaidi kuhusu programu hii na jinsi vijana wanavyoweza kuanzisha vikundi vya majadiliano ya mada mbalimbali kwa kutumia mwongozo wa FIKIA MAISHA, basi wasiliana na
Sales Manager wa Soma Biblia,
Mathayo Massawe
kwa namba ya simu +255 686 313 721 au
email: manager.somabiblia@gmail.com