YESU NI FIDIA - RIZIKI Toleo jipya
Anne Gihlemoen
“Badala ya - Maneno haya mawili ni “ufunguo” wa kufahamu mengi katika Biblia. Katika Biblia tunasoma kwamba kondoo mmoja alikufa badala ya Isaka. Na kule Misri, Waisraeli walipaka damu ya kondoo penye fremu za milango yao ili wazaliwa wa kwanza wapate kuishi. Yohana matizai alisema: Tazama, Mana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu. “Badala ya” ilikuwa mango wa Mungu, na kwetu ni habari njema.””
Manejo haya yameandikwa na Jon Jøssang, mwanzilishi wa gazeti la RIZIKI. Tarehe 30 mwezi Decemba 2016, aliitwa na Mungu mbinguni. Kwa hiyo toleo hili la RIZIKI limeandaliwa na makala maalumu, ili kukumbuka kazi ya Jon Jøssang.
Mwaka huu pia ni mwaka maalumu kwa ajili ya madhehebu ya kiprotestanti na hasa Kanisa la Kilutheri; 2017 tunasherekea maadhimisho ya miaka 500 ya Martin Luther kubandika hoja 95 kwenye lanzo la kanisa lake, tendo lililochangia sana kwa Matengenezo. Katika tolet hili la RIZIKI tutajifunza zaidi kuhusu maisha ya Luther na jambo moja la mana sana kwake, yaani, Yesu kama fidia; kifo cha Yesu "badala ya" mimi. Tunatarajia pia wewe utavutiwa na mambo haya.
Ukipenda kulipokea kila toleo la RIZIKI bure kwa njia ya posta au ya barua pepe, jiunga kwa kuweka comment hapo chini au kutuandikia kwa njia ya simu au barua pepe:
Simu: +255 752 379 932
Barua Pepe: editor.somabiblia@gmail.com
"Badala ya" inapatikana kwa maduka yetu yote.
Soma RIZIKI hapa https://issuu.com/riziki/docs/riziki_1_2017