Siku kuu ya watoto
Anne Gihlemoen
Watoto ni hazina kubwa kwa mzazi na kwa Kanisa-leo na kesho! Soma Biblia inapenda kufanya kazi ya kuhubiri Injili kwa watoto bega kwa bega na Kanisa. Kwa hiyo tunatoa ofa maalum kwa sharika zote zinazopenda kuwapa watoto wao zawadi kwaajili ya siku kuu ya watoto. Ni zawadi zinazodumu kwa muda mrefu, na zinawajenga watoto katika imani ya Kikristo.
Kwa wale watakao nunua Vitabu hivi kwa ajili ya sikukuu ya watoto tunatoa punguzo kwenye vitabu aina mbalimbali, ikiwa mtatoa maagizo na kulipa kabla ya tarehe 15/9/2017. Gharama ya kusafirisha vitabu kutoka Dar es Salaam, Iringa, Mbeya, Arusha na Mwanza ni juu yenu.
Mawazo mazuri kwa kupanga siku kuu ya watoto:
• Weka mipango mapema ili kuwa na uhakika kwamba siku kuu ya watoto itakuwa nzuri.
• Fikiri watoto wote mnapochagua zawadi. Mkipunguza gharama ya zawadi kwa ajili ya washindi watoto wote wanaweza kupewa zawadi nzuri.
• Jaribu kutafuta zawadi zinazodumu kama vitabu na majarida
• Kumbuka: Kwa njia ya watoto tunaweza kupata nafasi ya kuwafikia wazazi na ndugu wengine nyumbani kwao na habari njema ya Mwokozi wetu. Ikiwa watoto watapewa zawadi ya maandiko tutawafikia watu wengi pia.
JINSI YA KUAGIZA VITABU KWA AJILI YA SIKU KUU YA WATOTO
Utaratibu ni kuagiza vitabu unavyohitaji kwa njia ya kupiga simu au Barua pepe. Toa maelezo yafuatayo:
- Jina la kitabu na idadi unayohitaji.
- Njia ya usafirishaji (posta au basi).
- Jina lako, Anuani na namba yako ya simu.
Gharama ya usafirishaji utalipa kulingana na uzito wa mzigo, na njia ya usafirishaji. Baada ya kupokea agizo lako, tunapiga mahesabu ya gharama ya vitabu pamoja na usafirishaji. Ndipo tunakufahamisha gharama zote nawe utatueleza utalipa kupitia benki gani au m-pesa. Mara tukijua malipo yako yameingia katika akaunti yetu tunakutumia vitabu. (Mara nyingine inachukua muda wa siku mbili kabla malipo hayajaonekana katika akaunti yetu). Tutakapotuma mzigo wako tutakufahamisha ili uwe tayari kuupokea.
Soma Biblia , Dar es Salaam +255 754 292 995 dar.somabiblia@gmail.com
Soma Biblia, Mwanza +255 755 355 445 Mwanza.somabiblia@gmail.com
Soma Biblia, Iringa +255 765 910 495 Iringa.somabiblia@gmail.com
Soma Biblia, Arusha +255 766 615 746 Arusha.somabiblia@gmail.com
Soma Biblia, Mbeya +255 768 444 990 Mbeya.somabiblia@gmail.com