Ushuhuda wa Raphael Paul Kallaghe
Cathbert Msemo
“Bwana akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo. Akamwambia, Itupe chini; akaitupa chini, nayo ikawa nyoka; Musa akakimbia mbele yake. Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako, kamshike mkia; (akaunyosha mkono wake akamshika, naye akageuka kuwa fimbo mkononi mwake;)”
Nilikuwa sijui Neno la Mungu hivyo niliona kama nimepotoka na nikavutwa na kwenda upande mwingine. Namshukuru Mungu mama yangu mdogo alikuja na kunishuhudia akisema nilikuwa huko miaka mingi lakini nimeijua kweli na kweli ni Kristo na akanipeleke katika mkutano wa Injili. Napenda Neno hili la Kutoka 4:2-4 na nalitumia kufundisha vijana. Huu ni ushuhuda wa Raphael Paul Kallaghe mfanyakazi wa Soma Biblia Arusha. Ameeleza mengi ya maisha yake ya kuwa Mkristo. Karibu usikilize