Ushuhuda wa Irene Andrew Mwanjela
Cathbert Msemo
“1. Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2. Israeli na aseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
3. Mlango wa Haruni na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
4. Wamchao Bwana na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
5. Katika shida yangu nalimwita Bwana; Bwana akanijibu akaniweka panapo nafasi.
6. Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
7. Bwana yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa. ”
‘Kuokoka ni kuuishi Ukristo ni kumuishi Yesu. Kuokoka sio kuimba tu bali ni kuishi maisha halisi na Yesu’. Huu ni ushuhuda wa Irene Mwanjela mfanyakazi wa Soma Biblia Mbeya. Anaeleza vizuri jinsi alivyopita katika ngazi mbalimbali za ufahamu juu ya wokovu hadi kuelewa maana halisi na kuanza kuishi ndani yake. Karibu kusikiliza ushuhuda huu mzuri