Maisha ya Ebenezer Nelson Shafuri 'Mtu asiudharau Ujana wako'
Cathbert Msemo
“Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.”
Nilitafakari kupitia mstari huu wa 1 Timotheo 4:12 nikagundua kuwa kwa makundi niliyokuwa nayo ujana wangu ulikuwa unadharaulika. Lakini ukiwa na Yesu na kuacha baadhi ya mambo yasiyopendeza basi hakuna atakayekudharau. Ebenezer anasema haikuwa rahisi kwa wenzake kuelewa maisha yake mapya lakini jibu lake lilikuwa rahisi ‘Nimeamua kubadilika!’ Hatimaye wengine walitamani kuishi kama yeye. Karibu kusikiliza ushuhuda wa maisha ya kijana Ebenezer mfanyakazi wa Soma Biblia katika tawi la Arusha.