Joseph Nyngasa Mganga 'Ninamwamini na kumtegemea Yesu Kila wakati'
Cathbert Msemo
“Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile. ”
Kupitia neno hili, 2 Timotheo 1:12 nimejifunza kuwa katika maisha ya Imani kuna mateso, lakini ninachotakiwa kufanya ni kumwamini Yesu na kuendelea kumtegemea yeye kila wakati. Karibu kusikiliza ushuhuda wa maisha ya kikristo ya Joseph Nyangasa mfanyakazi wa Soma Biblia.