RIZIKI TOLEO LA 3, 2019 'TUNATAMBUAJE NAFASI YA WATOTO NA VIJANA NDANI YA KANISA?'
Cathbert Msemo
Vito vya thamani
Duniani kuna vito vingi vya thamani. Almasi ya Blue ni miongoni mwa madini ghali kuliko yote duniani. Bila shaka ukiwa na kipande cha almasi ya aina hii utakilinda sana.
Kanisa lina kitu chenye thamani zaidi. Lina watoto na vijana! Hawa ni kama mawe yaliyo hai katika nyumba ya Roho, na kama viungo katika mwili wa Kristo.
Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili namna ya kutambua nafasi ya watoto na vijana ndani ya kanisa. Nia ni kukumbushana kama kanisa umuhimu wa kuwatambua, ili tuwalee vizuri na kuwajali pamoja na vipaji walivyo navyo. Neno la Mungu linasema, “Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; kokote kigeukiapo, hufanikiwa” (Mit 17:8). Tutafute ‘kugeuza’ vito hivi vya thamani ndani ya kanisa vigeukie mwili wa Kristo!