TWENDE TOLEO LA 2, 2019 Linapatikana
Cathbert Msemo
MIMI NI WA YESU
Umewahi kusikia mtu akisema, “Mimi ni mwanafunzi wa Yesu”? Au, “Mimi ni mtoto wa Yesu? Au, “Mimi ni mtumishi wa Yesu? Je, ana maana gani hasa?
Soma makala za gazeti hili upate ufafanuzi mzuri kuhusu swali hili. Kwa mfano katika sala utajifunza jinsi Yesu alivyowaalika watoto kumfuata ili awabariki. Lakini wale aliokuwa nao wakataka kuwafukuza. Ilitokea nini mahali hapo? Yesu alisema, "Waacheni" tena akawaambia, "Ufalme wa Mungu ni wao".
Siyo kawaida mtu mwema kukaa na watu wenye tabia mbaya, sivyo? Lakini katika Hadithi utasoma kuhusu mtu fulani aliyeenda kushinda na kula nyumbani kwa mtu mwenye tabia mbaya ya kudhulumu mali za wenzie. Unafikiri huyu ni nani?
Kuna simulizi nzuri, katuni na ushuhuda wa mtu aliyempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wake miaka mingi iliyopita na hadi sasa anaitunza imani yake akimtumikia Mungu kwa kazi mbalimbali.
Twende ni kwa ajili ya Watoto na Vijana na linauzwa kwa bei poa ya Shilingi mia tano tu. Karibu dukani kwetu ujipatie nakala yako.
Bonyeza mkoa uliopo kupata mawasiliano: Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, Iringa, Mwanza