RIZIKI toleo la 02/2021 'Usitutie majaribuni, Utuokoe na yule mwovu' linapatikana
Cathbert Msemo
“Usitutie majaribuni, Utuokoe na yule mwovu”
Majaribu au kuingia katika majaribio, imekuwa jambo la kawaida katika maisha ya mwanadamu. Tangu mwanzo wa nyakati na hata leo hii, majaribu yamekuwa ni sehemu halisi ya maisha yetu ya kila siku. Jaribu linatajwa kama jambo la kawaida kwa wanadamu. Hii ina maana kuwa majaribu kwa watu wa Mungu au Wakristo si kitu kigeni. Pamoja na uwepo wa majaribu, Mungu ni mwaminifu kwetu. Ndiyo maana anaruhusu majaribu na pia kutupa mlango wa kutokea.
Ufafanuzi wa Sala ya Bwana unaendelea katika toleo hili la Riziki. Tumefikia sehemu ya nne, Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Mikononi mwa Mu-ngu majaribu yanaweza kuimarisha imani yetu na kutupa uzoefu kwamba Mungu ni mwaminifu na mwenye uwezo wa kutupitisha salama kiroho. Tunapopatwa na majaribu, kisha tukavuka salama, imani yetu huwa inaongezeka. Yesu anatuombea kila wakati; tulindwe na yule mwovu. Lengo la ombi hili ni kwamba, hata katikati ya majaribu, tulindwe dhidi ya hila za yule mwovu na tuvuke salama.
Ndani ya toleo hili utakutana na watu waliopita katika majaribu yaliyogusa kila eneo la maisha yao. Hata hivyo walisimama katika imani, na hatimaye walitoka wakiwa kama dhahabu safi ing’aayo. Siri yao ikoje? Soma makala za toleo hili, na ujifunze – kwa ajili ya maisha yako mwenyewe ili uweze kuwasaidia vema wanaojaribiwa!
Ukipenda kusoma kupitia RIZIKI ONLINE bonyeza HAPA