RIZIKI toleo la 1/2025 'Linapatikana'
Cathbert Msemo
Neema Yanitosha
Je, umewahi kujikuta katika hitaji kubwa la kuomba ulinzi wa gari lako kiasi kwamba ulitumia damu ya Yesu katika maombi yako? Wakati kama huo ulihofia nini? Na ulikuwa unaona nini mbele yako?
Katika maisha haya watu wengi wanatumia damu ya Yesu kwa mambo mengi. Lakini je, matumizi haya yote ni sawa?
Soma makala ya “Kwa damu ya Yesu” ili kutafakari swali hili zaidi.
Wakati viongozi wa kiyahudi walipompeleka Yesu kwa Pilato, na huyu aliona Yesu ni mwenye haki na hastahili kufa, walimjibu Pilato, “Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu” (Mt 27:25). Hili ni ombi baya sana, lakini hukumu hii ni tokeo lake ikiwa tunakataa matumizi halisi ya damu ya Yesu, yaani jinsi yeye mwenyewe alivyofanya upatanisho kwa njia ya kifo chake.
Soma pia makala kuhusu Paulo na anavyosema kwamba neema ya Mungu yamtosha. Ushuhuda huu hutokana na Paulo alivyoona kwamba damu ya Yesu inanena mema kuliko damu nyingine zote zilizomwagwa hapa duniani tangu Kaini alipomwua ndugu yake. Tumshukuru Mungu kwamba katika neema yake ametufungulia chemchemi ya kutakasa dhambi kwa njia ya damu ya Yesu.
Utapata pia kusoma mada kuhusu damu ya Yesu ilivyo na maana kwa ushirika wetu kama Wakristo, na ushuhuda wa kukutia moyo wakati unapoona ni kana kwamba Mungu hasikii maombi yako ya muda mrefu.